Offline
Fahamu wenyeji wa Kombe la Dunia 2030 na 2034
News
Published on 11/12/2024

Na RM

Alhamisi, Disemba 11, 2024

Uhispania, Ureno na Morocco wataandaa Michuano ya makala ya 25 ya Kombe la Dunia la FIFA ya Wanaume kwa pamoja ya mwaka 2030 wakati Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya makala ya 26 mwaka 2034.

Shirikisho la Soka Dunia FIFA lilidhibitisha katika Kongamano la FIFA baada ya kupiga kura.

Mataifa yote 211 wanachama wa FIFA yaliwakilishwa katika mkutano huo kwa njia ya video. Wenyeji wa michuano hiyo yote miwili walithibitishwa kupitia kura mbili tofauti.

Michuano ya mwaka 2030 itakuwa ni ya kuadhimisha miaka 100 ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia tangu ianzishwe kwa mara ya kwanza mwaka 1930.

Katika michuano ya mwaka 2030 pia kutachezwa mechi tatu nchini Argentina, Paraguay na Uruguay kuadhimisha miaka 100 ya michuano hiyo.

 

Comments
Comment sent successfully!